Vigezo na Masharti ya Mnada Poa


  UTARATIBU WA KUJISAJILI


 1. 1. Kabla ya Kuingia kwenye mnada tafadhali soma vingezo na masharti pamoja na kanuni za mchezo
 2. 2. Kwa msaada wa karibu usisite kuwasiliana nasi kwa namba yetu ya huduma au kupitia “chatbox” Hapo chini
 3. 3. Ili Kushiriki mnada unatakiwa kwa na miaka 18+, Usajili wako utakuwa Batili kama ikitambulika una umri chini ya miaka 18 na akaunti yako itafutwa kwenye mchezo huu wa MnadaPoa.
 4. 4. Ili kushiriki katika Mnada, unahitaji kutoa mahitaji halali kama nambari ya Simu Pamoja na Uhakiki wa mtandao husika wa simu utakaotumia kufanya malipo au kuweka salio kwenye akaunti yako.

 5. UTARATIBU WA BIDHAA ILIYO KWENYE MNADA

 6. 5. Mnadapoa haitawajibika kutoa au kufanya usajili wa bidhaa(GARI, PIKIPIKI nk) pia haitahusika au kuwajibika kusahihisha au kutoa uthibitisho wa vibali au leseni ambavyo vipo chini ya mamlaka husika
 7. 6. Mnadapoa itawajibika na gharama za uhifadhi wa bidhaa kabla ya kumkabidhi mshindi.Gharama zingine ambazo hazijaorodheshwa kama vile bima,usajili,vifaa na vinginevyo zitawajibika na mshindi mwenyewe.
 8. 7. Mnadapoa haitowajibika kwa tatizo lolote litakalotokea katika chombo kama vile kupotea au ajali iliyosababishwa na mshindi.
 9. 8. Mnadapoa haitowajibika kusikiliza malalamiko yoyote ambayo yatatolewa kuhusu bidhaa kwa niaba ya mshindi
 10. 9. Mnadapoa itawajibika endapo mapungufu ya bidhaa yatakuwa ndani ya sababu zetu.
 11. 10. Bidhaa au huduma zinazotolewa na Mnadapoa ni kwa ajili ya mshindi au mshiriki aliyeshinda.
 12. 11. Mshindi ataruhusiwa kubadilisha au kugawa bidhaa kwa mtu mwingine baada ya kuwa mmiliki halali wa bidhaa husika na MnadaPoa haitahusika na bidhaa hiyo baada ya makabidhiano kulingana na sheria za mchezo na kanuni zake.
 13. 12. Mnadapoa ina haki ya kubadilisha au kurekebisha bidhaa au huduma ya ofa wakati wowote bila taarifa ya awali kwa washiriki. Mnadapoa ina haki ya kuongeza muda wa kufunga mnada bila ilani ya awali kwa washiriki.
 14. 13. Picha za bidhaa zilizoonyeshwa kwenye tovuti sio picha halisi ya bidhaa yenyewe, Zimerekebishwa kwa kusudi la matangazo.
 15. 14. Hakuna bidhaa au huduma itakayobadilishwa kwa pesa au njia nyingine yoyote ya malipo na Mnada Poa.

 16. UPATIKANAJI WA MSHINDI

 17. 15. Ili dau liweze kushinda ni lazima liwe ni dogo na la kipekee wakati mnada unafungwa
 18. 16. Kama ikitoke madau yote yamegongana na hakuna dau la kipekee, basi mshiriki mwenye dau dogo kushinda wote na aliyetangulia kuweka dau lake atakuwa mshindi
 19. 17. Bodi ya Michezo ya kubahatisha Tanzania GBT itakuwa ndio yenye mamlaka ya mwisho kuamua mshindi wa Mnada
 20. 19. Muda wa mshindi kupokea zawadi yake kutategemea na umbali na taratibu za kiusafirishaji
 21. 20. Mshindi atatakiwa kushiriki kwa kufanya promosheni ya Mnada Poa kwa kupiga picha na video na hizo zitatumika kweny vyombo vya habari na sehemu nyingine mbalimbali kwa lengo la kuitangaza Mnada Poa.

 22. MATUMIZI MABAYA YA MNADA POA.

 23. 21. Katika Mnada Poa tunazuia kabisa watumiaji kufanya udanganyifu wa aina yoyote ile. Jaribio kama hilo linachukuliwa kama ukiukwaji wa sheria moja kwa moja.
 24. 22. Ifuatayo ni shughuli ambazo zimekatazwa kwenye Mnada Poa na hatua kali za kisheria zitachukuliwa zikivunjwa:
  • • Kupata, kurekebisha au kuharibu habari yoyote ya mtumiaji mwingine wa akaunti ya Mnada Poa kwa njia yoyote ya udanganyifu.
  • • Kujaribu kukusanya data kwenye tovuti au kwenye mitandao ya kijamii kwa matumizi binafsi.

 25. VIGEZO NA MASHARTI KWA UJUMLA

 26. 23. Mnadapoa ni mchezo unaohusisha uwekaji wa madau unaopima ustadi wa watu kuja na dau la kipekee kwa mapendekezo ya madau tofauti.
 27. 24. Dau la chini zaidi na la kipekee litatangazwa kama dau la ushindi mwisho wa mnada.
 28. 25. Baada ya kunukuu, imekubalika kuwa umesoma, kuelewa na kukubaliana na masharti na sera zote za mchezo huu.

 29. MAKUBALIANO YA MKATABA

 30. 26.Endapo utahitaji kutoendelea kupoke jumbe za matangazo kutoka Mnadapoa utawasilisha namba yako kwa kitengo cha huduma kwa wateja kupitia nambari ya simu 0659070070 au kupitia tovuti yetu ya www.mnadapoa.co.tz au kupitia kurasa zetu za mitandao ya kijamii za facebook au instagram ambapo kwa sasa ni @mnadapoa na huduma hio itasitishwa ndani ya masaa 24 ya kazi.Aidha ikitokea umeshiriki tena baada ya kutolewa kwenye huduma hio, utaendelea kupokea jumbe za matangazo kama awali hadi utakapo amua kujitoa tena.

 31. NENO LA SIRI

 32. 27. Tunza neno lako la Siri(password) kwa matumizi yako na usalama wa akaunti yako.Endapo utagundua matumizi mabaya ya akaunti yako tafadhali badilidha haraka neno lako la siri
 33. 28. Kumbuka neno la siri ndio namna pekee itakayokuwezesha wewe kutumia Tovuti ya MnadaPoa

 34. MATUMIZI YA DAU/SALIO

 35. 29. Dau lililoweka na mteja inapaswa kutumika ndani ya muda husika uliowekwa.Endapo muda wa dau kutumika utaisha pasipo kutumika, hakuna dau ama salio litakalorudishwa baada ya mnada kufungwa

 36. USITISHAJI MKATABA

 37. 30. Mnadapoa ina mamlaka ya kuzuia akaunti yako endapo utakiuka masharti ya matumizi ya tovuti ambayo yanaweza sababisha matumizi haramu ya tovuti ya Mnadapoa.

 38. SHIRIKI KWA SHERIA

 39. 31. Pindi unapojisajili na Mnada Poa, unatakiwa kufuata vigezo na masharti pamoja na kanuni za mchezo zilizowekwa
 40. 32. Madau yako yatakuwa batili kama utafanya au kushiriki kwenye mnada kwa kukiuka kanuni na makubaliano yaliyowekwa